Vituko na Vichekesho vya Mmasai na Mpogoro

0
28763
Soda ya coca cola

Kule Morogoro katika kibanda cha kuuzia vinywaji baridi kulitokea vichekesho vya mmasai mmoja na mpogoro mojawapo ya hivyo vichekesho hiki kidogo lakini inachekesha na kuvunja mbavu.

Kijana mmoja wa kimasai mtanashati, mwenye umri wa wastani alikwenda kujipatia kinywaji baridi katika kibanda hicho cha mpogoro.

Fuatilia mazungumzo yao:

Kijana wa kimasai alimsogelea muuza duka na kumuuliza

Kijana wa kimmasai: Ile soda nyeusi iko? (akimaanisha cokacola)

Muuza duka akifurahia kumpata mteja alijibu

Mpogoro muuza duka: Ndiyo ipo, karibu mteja

Wamasai kwa asili yao ni kama wakenya wengi hawaombi bali wanaagiza, kijana akaagiza soda hivi

Kijana wa kimmasai: Mpe mimi soda.

Kwa aharaka sana mpogoro muuza duka aliileta soda nyeusi na kumuambia

Mpogoro muuza duka: Hii hapa

Kijana wa kimmasai: Fungua

Mpogoro muuza duka: Nimeifungua hii hapa

Kijana wa kimasai akionyesha shilingi kumi alimwambia hivi

Kijana wa kimmasai: Nipimie ya silingi kumi, pesa hii hapa:

Mpogoro akaduwaa, sikujua kilichoendelea baada ya hapo

Leave your comment about Vituko na Vichekesho vya Mmasai na Mpogoro using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here