Vickekesho na Vituko vya Uzamiaji wa Kwenye Misiba

0
7621
Kituko cha uzamiaji wa kwenye misiba

Kituko cha uzamiaji wa kwenye misibaHapa duniani vituko haviachi kwisha, jamaa mmoja alitoa kichekesho cha mwaka katika moja ya uzamiaji wake wa kwenye misiba kutoka Arusha, siku moja katika pitapita yake aliingia mtaa mmoja na katika kutembea kidogo akakutana na nyumba yenye msiba.

Jamaa kama kawaida yake akazamia na kwa bahati nzuri akakuta ndo waombolezaji waliokuwa wamekesha hapo walikuwa wanapata uji wa moto ili kufukuza baridi. Jamaa naye yumo akapata kikombe chake na kwa bahati mbaya akapaliwa na uji wa moto kiasi cha kutokwa na machozi. Wale wenzake msibani wakaanza kumpa pole.

Ili kupotezea kwamba hajaunguzwa na uji akaanza kusema (huku akionekana analia kwa sababu ya yale machozi)

“MAREHEMU ALIKUWA MTU MZURI SANA” “YAANI ALIKUWA ANAPENDA WATU” “TAIFA LIMEPOTEZA TUNU MUHIMU SANA” “MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI”.

Kumbe aliyekuwa anazikwa ni katoto ka siku moja tu! Wazamiaji bwana!!

Leave your comment about Vickekesho na Vituko vya Uzamiaji wa Kwenye Misiba using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here