Wagombea Chadema Wadai Kunasa Kadi Feki za Mpigakura

0
360

Mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia , Saed Kubenea akionyesha kadi za kupigia kura jana zilizodaiwa kukamatwa hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa (Bawacha) ambaye pia ni  mgombea wa Kawe, Halima Mdee. Picha na Venance Nestory 

Kwa ufupi

Wadai za wakimbizi zimeingizwa kwenye daftari la wapigakura

By Raymond Kaminyoge, Mwananchi

Dar es Salaam. Wagombea ubunge wa majimbo ya Kawe na Ubungo kwa tiketi ya , wamedai kubaini kadi 100 za wapigakura ambazo hazina .

Walidai jana kuwa kadi hizo ni mpango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),  kujiandaa kuisaidia katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Kailima Kombwey alisema hafahamu kuhusu kadi hizo, huku akishauri suala hilo lipelekwe polisi ili waliohusika wakamatwe.

Akizungumzia madai hayo katika mkutano na wanahabari, mgombea wa Ubungo, Saed Kubenea alidai, “Hapa tunazo 100, lakini tume imeandaa kadi kati ya 2,000 hadi 3,000 ambazo zitatumika kuwaandikisha wapigakura wengine kwa lengo la kuisaidia .”

Aliwaonyesha waandishi wa habari kadi hizo, kisha kuziwasilisha kwa Wakili,  Frederick Kihwele aliyekuwapo katika mkutano huo.

Mgombea wa Kawe, Halima Mdee alisema uhakiki katika daftari la mpigakura unatakiwa kufanyika katika vituo vya kuandikisha kura badala ya kwenye ofisi za kata.

Alisema kata yenye watu 70,000, wananchi wake hawawezi kufanya uhakiki kwa siku nne zilizotolewa na NEC.

Mdee alidai kuwa wamepata kuwa wakimbizi 70,000 wameandikishwa kwa siri kwenye daftari hilo mkoani Kigoma.

Hata hivyo, Kombwey alisema hakuna mkimbizi aliyeandikishwa.

Akizungumzia siku za uhakiki katika daftari la mpigakura, Kombwey alisema suala hilo ni la kisheria na tume haiwezi kupingana nalo.

Leave your comment about Wagombea Chadema Wadai Kunasa Kadi Feki za Mpigakura using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here