Waislamu Hawataki Mahakama ya Kadhi Bali Sheria Zao Zitambuliwe

0
286

Mahakama ya Kadhi BungeniWAISLAMU HAWATAKI MAHAKAMA YA KADHI BALI SHERIA ZAO ZITAMBULIWE KISHERIA.

HII ELIMU HATA ASKOFU GWAJIMA ANGEPEWA ASINGEMTUKANA ASKOFU KARDINALI PENGO

Nimemsikia Kikwete mwenyewe, in fact sio mahakama ya Kadhi ndio Waislamu wanataka, wamekuja na “MISLEADING TITLE OF CLAIM”. Wanachotaka waislamu kutokana na ufafanuzi wa Rais ni sheria zao za ndoa na miradhi zitambuliwe na sheria ya nchi ili kule kwao Kadhi akitoa hukumu waliohukumiwa wasisepe bali watii kwa sababu ni sheria ya nchi kitu ambacho ilishakuwepo kwenye katiba tangu miaka ya 70 na sasa ni kuziboresha tu.

Kesi za jinai na zile za uhaini nk hazitahusu mahakama ya kadhi wala dini zingine bado zitakuwa chini ya Jamhuri.

Title ya madai yao haikukaa vizuri na ndio maana imepata upinzani mkubwa serikalini na kwa wasio waislamu. Mwanzo hata mimi nisie mwislamu niliogopa kwamba sasa mahakama ya Kadhi italeta mkanganyiko wa kisheria lakini ni sheria kutambuliwa kama ambavyo sheria za kikristo, kimila na dini zingine zinavyotambuliwa na zitaendelea kutambuliwa kwenye katiba na sheria za nchi. Kikwete amesema kuwa Waislamu watasimamia mahakama yao wenyewe, wakishindwa itakuwa juu yao, serikali haitahusika.

Kwa hiyo kama Muswaada ulio bungeni ambao ndio utajadiliwa na wanataka mahakama ya Kadhi itambuliwe mimi siungi mkono kwani kutaleta mkanganyiko wa ksiheria lakini kama ni selected laws ambazo hazikinzani na sheria mama ya nchi mimi sina shida nayo na nadhani hii elimu hata Askofu Gwajima angepewa asingemtukana Askofu Kardinali Pengo

Leave your comment about Waislamu Hawataki Mahakama ya Kadhi Bali Sheria Zao Zitambuliwe using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here