Wanafunzi 29 Waalimu 2 na Dereva 1 Wafariki Katika Ajali Mbaya Karatu, Tanzania

0
113


?Ajali mbaya ya gari imetokea kule Karatu, Arusha kwa kuhusisha basi dogo aina ya Costa inayomilikiwa na shule ya Lucky Vincent iliyoko KwaMrombo, kusini mwa jiji la Arusha. 

Basi hilo limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, Karatu jana wakiwa kwenye ziara ya kimasomo kwa shule rafiki ya Tumaini English Medium Junior Schools ili kufanya mtihani wa kanda wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba wa Kanda.


?Eneo ajali ilikotokea liko takribani kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro  na kama kilomita 150 kutoka mjini Arusha.

Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mwalimu ilisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi na waalimu wanaosadikiwa kuwa thelathini na tano.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mvua kali inayoendelea kunyesha katika eneo hilo. Waliendelea kudai kuwa pia dereva ni mgeni na hakujua njia hiyo kuwa ikinyesha huwa inautelezi sana. Basi liliteleza na kukosa mwelekeo na kutumbukia korongoni katika mto Malera.


?Taarifa kutoka hospitali ya Lutheran Karatu, zinadai kuwa maiti zilizopokelewa ni 32.  Waalimu wawili (2), dereva mmoja (1), na wanafunzi ishirini na tisa (29).

Idadi ya wanafunzi waliofariki ni 10 wa kiume na 18 wasichana.

Orodha ya majina ya wanafunzi waliofariki imeambatanishwa hapa?Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fabian Dagalo imewataka wananchi kuwa watulivu wakati huu wa maombolezo na kwamba serikali itatoa taarifa kamili ya msiba huo baadaye.

Mhe. Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma jana salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo na kueleza kuwa ajali hiyo imezima ndoto ya watoto hao waliokuwa wakijiandaa kulitumikia Taifa na kudai kuwa ajali hiyo imeacha uchungu, huzuni, na masikitiko makubwa kwa familia na Taifa kwa ujumla. 

Barua ya rambirambi iliyoandikwa na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu kwa niaba ya Rais imeambatanishwa hapa


?

Leave your comment about Wanafunzi 29 Waalimu 2 na Dereva 1 Wafariki Katika Ajali Mbaya Karatu, Tanzania using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here