Wananchi Wachoma Basi la Mtei Singida Kimakosa

0
1399
Basi la Mtei lachomwa moto

Taarifa za abiria walikuwa kwenye basi la Mtei inasema kuwa basi hilo lililopata ajali na kuua watoto wawili wa familia moja baada ya basi hilo kumgonga mwendesha bodaboda ambaye aliwabeba watoto hao.

Taarifa zinaendelea kutabainisha kuwa mwendesha bodaboda huyo aliingia barabara kuu bila kuchukua tahadhari na kukutana na basi hilo ambalo baada ya kumgonga mwendesha boda boda lilimburuza pembeni mwa barabara.

Watu bila kuuliza walilishambulia basi hilo na kuliteketeza kwa moto kama linavyoonekana kwenye picha.

Haya ndio madhara ya kujichukulia hukumu na sheria mikononi kwani basi halina hatia yoyote sasa limechomwa moto. Inasikitisha pia kwani mabegi na mali za abiria zilizokuwamo ndani ya gari vyote vimeteketezwa kwa moto.

Basi la Mtei lachomwa moto na watu wenye hasira
Basi la Mtei baada ya kuteketezwa kwa moto abiria wake wakiwa nje ya basi

Nawapa pole wote walifikwa na msiba huu mkubwa wa kuondokewa na watoto wawili kwa mpigo.

Watanzania hasa wazazi tufunguke macho tusiwaweke watoto wetu rehani kwa kuwapa wabeba mishikaki na kuhatarisha uhai wa wapendwa wetu.

Bodaboda iliyogongwa na basi la mtei na kuua watoto
Pikipiki iliyowabeba watoto wawili ambao walikufa kweny hiyo ajali

Chondechoinde Watz tubadilike na tuwapende zaidi watoto wetu tusiwatoe mikononi mwa watu wasio salama.

Basi la Mtei lililochomwa moto na watu wenye hasira
Basi la Mtei lililoteketea kwa moto likiwa na abiria wake, mabegi na mizigo yote yaliteketea pia kwa moto

Leave your comment about Wananchi Wachoma Basi la Mtei Singida Kimakosa using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here