Wizi unaofanywa na Makampuni ya Simu Tanzania

2
460

Makampuni takriban yote yanayotoa huduma za pesa kwa njia ya elektroniki (hasa ya Makampuni ya simu na mabenki) huwaibia wateja wao pesa nyingi bila wao kujua

Teknolojia mpya haiji tu na faida kwa watumiaji, hasa katika kumuokolea mtumiaji muda lakini pia huja na hasara ya kuibiwa pesa nyingi bila ya mtumiaji kujua

Mfano

  1. Wizi wa kawaida  kwa njia ya mtandao
  2. Wizi kwa njia ya makosa ya kiufundi
  3. Wizi kwanjia ya huduma zisizotakiwa na mteja
  4. Nk

Nielezee tu mfano wa wizi kwa huduma ambazo mteja hakuzitaka (Hasa interneti matumizi nje ya vurushi za kununua)

Airtel wanatoa iterneti ya bure usiku

ukitumia mpaka saa 12 kamili asubuhi, baadaya ya hapo utachajiwa Tsh 100 kwa kila MB utakayoitumia
Hivyo hivyo ukinunua bundle
Vodacom nao ukinunua bundle halafu ikaisha unaunganishwa na huduma ua interneti ya out of bundle service ambayo hukuitaka na unachajiwa Tsh 154 kwa kila MB utakayoitumia
TIGO wao wanaiba nusu ya Airtel, Ukutumia bundle uliyoinunua halafu ikaisha, utaunganishwa na huduma ya out of bundle ambayo hukuitaka utakayochajiwa Tsh 50 kwa kila MB

Hoja yangu ni hii

Hizi out of bundle zinaunganishwa bila ya wewe kuulizwa au kuomba. na unakatwa mapesa kibao

Hebu jaribu kufuatilia huu mfano wa pesa kila mtu anakatwa

ProviderOut of bundle Price/MBPossible MB Overuse/DayAmount/Year/userSample of 100000 Users Amount Stolen
Vodacom15450              2,810,500.00              100,000.00                     281,050,000,000
Airtel10050              1,825,000.00              100,000.00                     182,500,000,000
TIGO5050                 912,500.00              100,000.00                        91,250,000,000
                     554,800,000,000

Zaidi ya milioni 500 huibwa kila mwaka na makampuni ya simu za VodaCom, Airtel na Tigo pekee kwa wastani wa watumiaji wa internet 300,000 kote nchini

Leave your comment about Wizi unaofanywa na Makampuni ya Simu Tanzania using the comment form below

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here